Wilehadi wa Denmark

Wafiadini wa Gorkum walivyochorwa na Cesare Fracassini (1838-1868), Vatikani.

Wilehadi wa Denmark (1482 - 1572[1]) alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo kutoka Denmark aliyefia imani ya Kikatoliki huko Uholanzi pamoja na wenzake 18 maarufu kama Wafiadini wa Gorkum[2].

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini. Kwanza alitangazwa na Papa Klement X kuwa mwenye heri tarehe 24 Novemba 1675, halafu mtakatifu na Papa Pius IX tarehe 29 Juni 1867.

Sikukuu yake na ya wenzake huadhimishwa tarehe ya kifodini chao, 9 Julai[3].

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/99249
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/93406
  3. Martyrologium Romanum

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search